Environmental Action Network Tanzania, inaelekea kwenye kilele cha kutimiza miaka 3 tangu kuanzishwa kwake, hivyo inapenda kushiriki pamoja na wanafunzi kupitia shindano.
Nifanye niwe rafiki ni mpango wa kubadili chupa za plastiki kufanyika kuwa moja ya nyenzo muhimu katika kazi mbalimbali za mwanadamu. Nifanye niwe rafiki ni sehemu ya kwanza ya shindano letu namba tatu.
SIFA ZA WASHIRIKI: Mwanafunzi yeyote mwenye akili timamu na mwenye umri kuanzia miaka 13 na 20. mwanafunzi atatakiwa kuandika Jina lake Kamili, Shule anayosoma, Kidato anachosoma, Mwalimu wake msimamizi.
LENGO LA SHINDANO: Plastiki ni aina ya taka ngumu inayoshamiri kuzagaa ovyo kwenye mazingira yetu na ni moja ya taka hatarishi kwa sasa kwa mazingira yetu. Lengo kuu ni kuibua kazi mpya za chupa za plastiki zilizokwisha kutumika ili zitumike upya kwa kazi nyingine tofauti na ya awali, au kuendeleza matumizi zaidi ya chupa za plastiki katika matumizi ya shughuli za binadamu za kila siku.
MUDA WA SHINDANO: Shindano litaanza rasmi tarehe 24.04.2018 hadi tarehe 01.05.2018.
ZAWADI: Zawadi kwa washiriki wote zitatolewa, ila kutakuwa na zawadi maalum kwa washindi watatu wa kwanza.
#JIPANGE.
NAMNA YA KUSHIRIKI: Mshiriki atatakiwa aandae andiko fupi(lisilo pungua kurasa tatu) linalo ezea madhara ya taka zitokanazo na plastiki, ni kwa namna gani mshiriki hushiriki kupunguza uzalishaji wa taka aina hiyo na ni kwa namna gani taka aina ya plastiki (chupa za plastiki) zinaweza kuwa na kazi mbadala.Andiko hilo liwasilishwe kwa Mwalimu wako ili aweze kulituma kwenye email:ipyana78@gmail.com kabla ya tarehe 03.05.2018 saa 6 kamili mchana.
ANGALIZO: Kwa mwalimu mwenye dhamira ya dhati kwa wanafunzi wake kushiriki, uongozi unaomba tuwasiliane haraka iwezekanavyo ili kuwapa nafasi wanafunzi wengi zaidi kushiriki zoezi hili. Pia Uongozi unaomba mtoe taarifa kwa wakuu wenu wa shule kuhusu kuwepo kwa shindano hili.
Imetolewa na:
Environmental Action Network Tanzania
Go Clean,Go Green
+255713852483
Mabibo - Dar es Salaam & Mapinga-Bagamoyo
23rd April, 2018




0 comments:
Post a Comment